Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

TFRA Logo
TFRA Kanda ya kati yaja na mashamba darasa kuhamasisha matumizi sahihi ya mbolea
22 Mar, 2024 08:00-15:30
TABORA
PR

Katika kuhakikisha Sekta ya Kilimo inatimiza azma yake ya Agenda 10/30: Kilimo ni biashara kufuatia tija ipatikanayo kutokana na shughuli za kilimo Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imeendelea kubuni mbinu za kuhakikisha wakulima wanazingatia kanuni bora za kilimo.

Hayo yamebainika kufuatia uanzishwaji wa mashamba darasa wilayani Nzega Mtaa wa makalome kata ya ijanija uliofanywa na Ofisi ya Mamlaka Kanda ya Kati kwa kushirikiana na wadau wengine wa kilimo.

Akiwataja wadau hao, Kaimu Meneja wa TFRA Kanda ya kati, Allan Mariki amesema ni kampuni za mbolea za ETG na Minjingu pamoja na Wakala wa Mbegu ASA.

Uanzishwaji wa Mashamba hayo umefanyika tarehe 21 Machi, 2024 ambapo mazao ya mahindi na alzeti yatatumika kuhimiza juu ya matumizi sahihi ya mbolea pamoja na kuzingatia kanuni zote za kilimo ikiwemo kuandaa mashamba kwa wakati, kupanda kwa mbolea, kupalilia na kukuzia mazao yao kwa wakati.

Agenda ya serikali ifikapo mwaka 2030 ni kuongeza mchango wa Sekta ya Kilimo kwenye pato la taifa kwa asilimia 10.

TFRA Kanda ya kati yaja na mashamba darasa kuhamasisha matumizi sahihi ya mbolea