Wakulima wa kijiji cha Makowo mkoani Njombe wakifuatilia elimu ya matumizi sahihi ya mbolea inayotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania( TFRA) , yenye lengo la kuwajengea uwezo wakulima kwenye uchaguzi wa mbolea za kupandia, kukuzia na kuzalishia ili kuongeza tija ya uzalishaji.
Afisa Udhibiti Ubora wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Henerico Renatus akitoa elimu ya Matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima wa kijiji na Kata ya Makowo mkoani Njombe, tarehe 2 Oktoba, 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent, akihamasisha wakulima wa Kijiji cha Makowe kuhusu uzingativu wa matumizi sahihi ya mbolea katika kuongeza tija ya uzalishaji msimu wa kilimo 2025/26 tarehe 2 Oktoba, 2025