Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary T. Mgumba atembelea Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA)

Naibu waziri wa kilimo Mh. Omary Mgumba asisitiza utendaji wa haki na weledi katika tasnia ya mbolea nchini ili kukuza sekta ya kilimo na kuongeza uzalishaji na tija ili kuchochea maendeleo ya viwanda na pato la mkulima. Naibu Waziri aliyasema hayo alipotembelea Ofisi za Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe. Mgumbo na watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania TFRA

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Mgumba na watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania

Mhe. Mgumba aliyasema hayo baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania toka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Lazaro Kitandu.

Naibu Waziri Mh. Mmgumba pia alisisitiza Mamlaka kuweka mkakati madhubuti kuhakikisha elimu ya matumizi bora ya mbolea inawafikia wakulima ili kuongeza tija katika kilimo na kuweka wakulima katika ushindani wa biashara ndani na nje ya nchi.

Mh. Mgumba alielekeza Mamlaka kuwa na mpango mkakati wa kutekeleza ASDP II katika mapinduzi ya kilimo, kuongeza uzalishaji na tija, Pia Naibu Waziri alisisitiza uhalisia wa takwimu na vipaumbele viwe vya ukweli na uhakika kuepusha hasara na kutofanikiwa kwa mipango endelevu kunakoweza kusababishwa na takwimu na vipaumbele visivyo na uhalisia au usahihi.

Contact Details

TANZANIA FERTILIZER REGULATORY AUTHORITY
Mandela Road, Temeke Veterinary.
Ministry of Livestock and Fisheries
Former PADEP Building
P.O Box 46238,
Dar Es Salaam,
Tanzania
Tel: +255 22-2862595
Mobile: +255 710107631
E-mail: info@tfra.go.tz